✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 3: Siri ya Binamu Dora

Macho ya Robby yalikuwa yamejaa chuki. Alinikaribia huku akitafuna jani la mti fulani, ishara ya dharau iliyopitiliza. "Tom, unadhani kumuiba mwanamke Dar ni sawa na kumuiba kuku wa kienyeji kijijini kwenu? Lisa ana mwenyewe, na mwenyewe ni mimi."

Nilitabasamu kiume. "Robby, mwanamke hadiliki kwa maneno ya vijiweni. Kama Lisa ni wako, mbona dakika tano zilizopita alikuwa mikononi mwangu akilia kwa huba?"

Kauli hiyo ilikuwa kama petroli kwenye moto. Robby alipiga hatua moja mbele, lakini kabla hajarusha konde, simu yake iliita. Aliiangalia, akatazama sura yangu kwa hasira, kisha akatema mate chini. "Hii mechi haijaisha, Tom. Utajua kwanini naitwa Robby wa Mwenge." Aligeuka na kuondoka na wapambe wake.

Nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo mawili. Lisa alikuwa hatarini, na Caroline alikuwa anaanza kuniteka. Nilipoingia ndani, nilimkuta **Dora**, binti wa mjomba wangu tunayeishi naye, akiwa amejipumzisha sebuleni. Alikuwa amevaa kanga moja iliyokuwa imefungwa kiholela, ikionyesha miguu yake minene iliyopakwa mafuta ya nazi yakang'aa.

"Shemeji umerudi? Mbona umekuja na uso wa mbuzi?" Dora aliniuliza huku akijinyoosha, kanga ikalegelea kifuani.

"Dora, nimechoka na hizi kanga zako. Unajua kabisa Lisa hapendi kukuona hivi unavyonizunguka," nilimjibu huku nikijaribu kukwepesha macho.

Dora alicheka kicheko cha kilevi, ingawa alikuwa hajalewa. "Lisa? Huyo binti wa kishua anayekupa dakika tano tu? Tom, mimi nipo hapa saa ishirini na nne. Mimi ndiye ninayejua unapenda kula nini, mimi ndiye ninayefua nguo zako. Lisa anakupa maneno, mimi nakupa huduma."

Alinisogelea na kunishika bega. Harufu ya manukato yake ya bei rahisi ilichanganyika na joto la mwili wake. "Unajua Tom, kuna siri moja kuhusu huyo Lisa wako ambayo huijui. Robby amekuwa akija hapa kila mara ukiwa shule kumuulizia Lisa. Na cha ajabu, Lisa amekuwa akimtumia ujumbe wa siri kupitia simu yangu."

Moyo ulinituma kumzaba kofi, lakini uzoefu ulinizuia. "Unasema nini Dora? Lisa anamtumiaje Robby ujumbe?"

"Dora hadanganyi, Tom. Lisa anajua mimi na wewe tuko karibu, hivyo anatumia namba yangu kuongea na Robby ili wewe usigundue kwenye simu yake. Wanapanga kukuacha solemba siku utakayomaliza masomo," Dora aliniambia huku akinitazama kwa huruma ya kinafiki.

Nilijisikia kama nimepigwa na radi. Je, Lisa yule aliyekuwa ananiangalia kwa macho ya huba dakika chache zilizopita alikuwa msaliti? Au Dora alikuwa ananitega ili amtoe Lisa mchezoni na yeye achukue nafasi yake?

Nilikimbilia chumbani kwangu na kujifungia. Niliichukua simu yangu na kukuta ujumbe wa Caroline: *"Tom, mbona umeninyamazia? Nimekuandalia zawadi ndogo kesho ofisini ukija kuleta mwamvuli wangu."*

Niliutazama ule ujumbe, kisha nikaangalia picha ya Lisa niliyoiweka kama *wallpaper*. Machozi yalianza kunilengalenga. Nilikumbuka kiapo chetu cha damu tulichokifanya tukiwa Tabora. Je, damu ile ilikuwa imeshapoteza nguvu?

Ghafla, mlango wa chumba changu ulifunguliwa taratibu. Alikuwa Dora. Aliingia ndani na kufunga mlango kwa ufunguo. "Tom, achana na wasaliti. Mimi nipo hapa kwa ajili yako usiku wa leo."

Nilitaka kumfukuza, lakini ule "Uzoefu" wa shetani uliniambia, "Kama Lisa anakusaliti na Robby, kwanini wewe usile tunda lililo mbele yako?"

**ITAENDELEA SEHEMU YA 4...**