✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 6: Mvurugiko wa Mwili na Shaka ya Mume

Wiki mbili zilipita kwa kasi ya ajabu, zikiwa zimetawaliwa na maisha ya siri na ya hatari sana. Kila Jumanne na Alhamisi, nilijikuta nikirudi kwenye kile chumba namba 304 cha hoteli, ambapo Baraka alikuwa ananichakata kwa mikwaju mizito ya dhati na ya kila namna. Mwili wangu ulikuwa umeshazoea ile dozi yake, na kila tukimaliza, nilikuwa nameza kile kidonge cha dharura (P2) kama peremende, nikiamini ndio ngao yangu pekee dhidi ya dhoruba inayoweza kunisomba.

Wakati huohuo, nyumbani mambo yalianza kubadilika. Dozi ya vidonge na sindano za homoni alizopewa mume wangu kule hospitali zilianza kufanya kazi kwa kasi kubwa. Macho yake yalianza kurudiwa na uchangamfu, na hata ule unyonge na uoga wa kiume ulikuwa unamfuta taratibu. Alianza kunishika viuno asubuhi, na kila akinitazama, niliona ule uchu wa mwanaume anayetaka kurudi kwenye uwanja wake wa dhati.

Hata hivyo, katikati ya mabadiliko hayo mazuri ya mume wangu, mwili wangu mimi ulianza kunisaliti.

Ilikuwa ni asubuhi ya Jumatano, nikiwa nimesimama mbele ya kioo cha bafuni nikisafisha kinywa changu kwa umakini mkubwa kama ilivyo tabia yangu ya usafi. Ghafula, nilihisi wimbi zito la kizunguzungu likipanda kutoka tumboni hadi kichwani. Mate yalianza kujaa mdomoni kwa kasi, na kabla sijaelewa nini kinaendelea, nilijikuta nanyamaa juu ya sinki na kuanza kutapika pua na mdomo.

"Mke wangu! Kuna nini?" Mume wangu alisukuma mlango wa bafuni na kuingia kwa dharura, uso wake ukiwa umejaa wasiwasi. Alianza kunisugua mgongo kwa upole huku mimi nikiendelea kutoa nyongo ya njano.

"S-sijui mume wangu... nahisi kichefuchefu kikali sana tangu nimeamka," nilisema kwa sauti ya kinyonge, nikisukutua mdomo wangu kwa maji ya baridi na kupangusa uso.

Mume wangu alinitazama kwa jicho la uchunguzi sana, jicho ambalo lilifanya moyo wangu uanze kupiga dundo za hofu. "Kichefuchefu? Mbona kama dalili za... Hapana, hebu subiri. Najma, mara yako ya mwisho kuingia kwenye siku zako (hedhi) ilikuwa lini?"

Swali lile lilikuwa kama radi iliyopiga ndani ya bafuni lile. Nilishikilia ukingo wa sinki, nikijaribu kukumbuka. Kwa kawaida, mimi ni mwanamke msafi na nina kalenda yangu ya hedhi kichwani. Nilipopiga hesabu, niligundua kuwa nilikuwa nimepitiliza siku zangu kwa wiki nzima sasa! Yale makombora ya vidonge vya P2 niliyokuwa nameza kila baada ya mikwaju ya Baraka yalikuwa yamevuruga kabisa mfumo wangu wa homoni na kuzuia hedhi yangu isiende kwa wakati.

"M-mume wangu... mbona mwezi huu sijaingia kabisa," nilijibu kwa sauti ya chini, macho yangu yakitazama chini ili asisome hofu iliyokuwa inatishia kuniliza.

Mume wangu alirudi nyuma hatua moja, sura yake ikabadilika na kuwa ngumu, yenye mchanganyiko wa maswali mengi. "Hujaingia hedhi, na una kichefuchefu cha asubuhi? Najma, unajua maana yake?"

"Mume wangu, inaweza ikawa ni mabadiliko tu ya hali ya hewa au stress za ofisini," nilijitahidi kujitetea, lakini sauti yangu ilikuwa inatetemeka.

"Stress gani inazuia hedhi na kuleta kichefuchefu cha kutapika, Najma?" Mume wangu alisema, sauti yake ikianza kupanda upole wake wa siku zote ukatoweka. Alinyosha mkono wake na kushika mabega yangu, akinitazama machoni kwa ukali ambao sijawahi kuuona kwake kwa miaka 14. "Kumbuka majibu ya daktari wiki mbili zilizopita! Mbegu zangu ziko SIFURI. Siwezi kutoa mimba kwa sasa hadi dozi yangu iishe baada ya miezi mitatu. Kama wewe una mimba sasa hivi... ni ya nani, Najma? Kuna mwanaume mwingine anakuingilia nje?"

"Hapana mume wangu! Wallah nakunyoshea mikono, hakuna mtu mwingine!" Nilipiga magoti hapo hapo bafuni, machozi yakinitoka kwa kasi. Usafi wangu na uaminifu wangu wa miaka yote vilikuwa vinatumika kama kinga ya uongo. "Unajua jinsi gani najitunza, unajua usafi wangu na jinsi navyokupenda! Unawezaje kunihisi hivyo mume wangu?"

Mume wangu alishusha pumzi ndefu, akajiondoa mkononi mwangu na kutoka chumbani bila kusema neno lingine. Aliondoka kwenda kazini kwake akiwa ameacha ukuta wa mashaka makubwa ndani ya nyumba yetu.

Nikiwa bado nimekaa chini pale bafuni nkilia, nilichukua simu yangu kwa mikono inayotetemeka. Nikamwandikia Baraka ujumbe:

*"BARAKA, MAMBO YAMEHARIBIKA! Sijaingia hedhi, natapika asubuhi na mume wangu ameshaanza kunihisi usaliti kwa sababu anajua hawezi kutoa mimba! Nipo kwenye dhoruba kali mno sasa hivi!"*

Baada ya dakika mbili, Baraka alipiga simu. Sauti yake haikuwa na hofu kabisa, ilikuwa na ule ule utulivu wa hatari.

"Najma, tulia. Hiyo ni athari ya vile vidonge vya P2, vinavuruga mzunguko lakini havishiki mimba. Nataka uje ofisini kwangu mchana huu, nina mpango utakaomfanya mumeo afunge mdomo wake kabisa na aamini kuwa mimba hiyo—kama ipo—ni ya kwake. Njoo sasa hivi."

---

**Katika Episode inayofuata:** Najma anaenda ofisini kwa Baraka na kupewa mbinu ya hatari sana ya "kumtega" mume wake usiku huo huo ili mume aamini kuwa amerudisha uwezo wake wa kiume na kumpa mimba yeye mwenyewe. Je, mtego huo utafanikiwa? Usikose **EPISODE 7: Mtego wa Kitandani na Akili ya Mume wa Nje**.