✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 16: KISASI CHA PETROLI NA MOTO WA GETINI

Harufu ile nzito ya petroli ilipozidi kuingia puani, mwili wangu wote ulisisimka kwa uoga. Niliacha kutazama lile lori la Grace lililokuwa linaondoka, nikakimbilia mlangoni na kuchungulia kwa siri kupitia tundu la kitasa cha mlango wa mbele.

Macho yangu yalikumbana na mnyama wa mjini aliyepandisha wazimu. Alikuwa ni Irene! Alikuwa amevaa ushungi mweusi uliofunika kichwa chake ambacho hakikuwa na wigi tena baada ya kuraruliwa na Grace, na mikononi mwake alikuwa ameshikilia dumu la lita tano la petroli akilipasua kwa fujo juu ya milango na madirisha ya mbao ya nyumba yangu. Sura yake ilikuwa imepinda kwa roho ya kikatili, akisema kwa sauti ya chini ya kisasi, *"Linda malaya wewe, uliona siri yangu kuwa wazi ni mchezo? Leo nakuunguza humu humu ufe ukiwa uchi!"*

Kabla sjamwambia neno lolote, Irene alichomoa kiberiti mfukoni mwake, akawasha njiti moja na kuitupa juu ya ile petroli.

*Fuuuuuuuup!* Moto mkubwa wa bluu na njano ulilipuka mara moja, ukasogea kwa kasi ya ajabu kukamata pazia za madirisha yangu na kuingia ndani ya sebule. Moshi mzito mweusi ulianza kutanda chumbani kwangu, ukiziba hewa na kunifanya nianze kukohoa kikatili, *“Khoo! Khoo! Jamani motoooo! Irene unaniuaaa!”*

Nilichanganyikiwa vibaya mno. Mlango wa mbele ulikuwa unawaka moto wa radi, na singeweza kupita. Niligeuka mbio nikiwa uchi wa mnyama, nikakimbilia kule mlango wa nyuma niliouzoea kupitishia wanaume. Niliufungua kwa haraka, nikajitupa nje kwenye kile kichochoro cha nyuma huku nikiwa niko tupu kabisa, sina hata kanga ya kujifunika mwili wangu uliokuwa bado unanukia jasho la Saimoni wa mchana ule.

Kelele zangu na ule moshi mkubwa uliokuwa unafuka ulimfanya Saimoni, ambaye alikuwa bado yuko peke yake chumbani kwake baada ya Grace kuondoka, atoke mbio uani mwake. Aliponiona nimesimama kule uani kwangu nalia huku niko uchi wa mnyama na nyumba inateketea, alishtuka vibaya mno.

"Linda! Kuna nini jirani? Nyumba inawaka?!" Saimoni alipiga yowe, akisogea haraka kwenye ule ukuta wetu mdogo wa fensi.

"Saimoni niokoe! Irene amemwaga petroli anataka kuniua humu ndani!" nililia kwa sauti ya kukatika, moshi ukiwa unaninyonga koo.

Saimoni alipoona vile, licha ya fujo zilizotokea, hakutaka kuona mwanamke aliyempa utamu masaa machache yaliyopita akiteketea. Aliruka ule ukuta kwa fujo ya kiume, akazama ndani ya uwanja wangu, akavua lile shuka la kitanda lililokuwa limeanikwa kwenye kamba akanivurusha mziki mzima mwilini mwangu ili kuficha aibu yangu mbele ya majirani walioanza kukimbilia upande wa mbele kuzima moto.

"Twende kwangu Linda, haraka!" Saimoni aliamrisha, akonishika mkono uliokuwa unatetemeka na kunivuta upande wa kwake, huku nyuma yetu nyumba yangu ikizidi kuliwa na miali ya moto wa kisasi cha Irene.

Tulipotua sebuleni kwake, mazingira yalikuwa matupu kwa sababu Grace alishaondoka na kila kitu. Kitanda pekee ndicho kilichokuwa kimebaki chumbani. Saimoni alinilaza juu ya kile kitanda chake cha ndoa kilichokuwa wazi, akajifungia mlango wa chumba hicho kwa ufunguo mtaa usije kutuona.

Mwili wangu ulikuwa unatetemeka kwa hofu ya kifo nlichokiokoka, lakini jinsi Saimoni alivyokuwa ananitazama akiwa amesimama mbele yangu, niliona macho yake yakibadilika tena. Hofu ya moto iliamsha ashiki nyingine ya ajabu ya kinyama ndani yetu sote wawili. Tulikuwa katikati ya janga kubwa la mtaa, lakini miili yetu ilikuwa na kiu isiyoisha!

---

**Utangulizi wa Episode Inayofuata (EPISODE 17: PENZI LA KWENYE MAJIVU):**
Linda na Saimoni wanajikuta wakizama kwenye mechi nyingine ya fujo kubwa chumbani kwa Saimoni wakati nyumba ya Linda ikiwa bado inateketea kwa nje. Lakini wakati wakifikiri wako salama na siri yao mpya ya kifo, mtu mmoja wa karibu anakuja kugonga mlango wa chumba hicho usiku akitafuta hifadhi baada ya tifu la moto kuisha. Usikose **EPISODE 17** inayofuata, mambo yanazidi kuwa magumu!