โœฆ Matangazo โœฆ

๐Ÿ“– Story Tamu

Episode 5: Mtego wa Wiki Mbili Mbele

Zile wiki mbili zilizofuata zilikuwa ndefu na zenye mateso makali kwangu. Kelvin alikuwa kimya kabisa; hakuna ujumbe wa asubuhi wa kuniita "mdogo wangu mrembo," wala simu za kibiashara. Kila dakika niliyotazama skrini ya simu yangu bila kuona jina lake, nilihisi upweke mkali ukitafuna roho yangu.

Kibaya zaidi, hali yangu ya kiuchumi ilianza kuyumba kwa kasi. Pesa za matumizi nilizokuwa nimezoea kuzipokea kutoka kwake zilikata, na hapo ndipo nilipotambua jinsi Kelvin alivyokuwa nguzo muhimu kwenye maisha yangu.

Kitandani, mambo yalikuwa magumu zaidi. Zile sekunde mbili alizonijibu lile busu zikawa ndio wimbo wangu wa usiku. Nilijikuta nikijipapasa mwili mzima gizani, nikivuta picha ya mikono ya Kelvin ikiwa kiunoni mwangu, nikiguna kwa sauti ya chini kwa hamu na uchu wa mwanaume huyo, nikiamini kabisa kuwa ukimya wake unatokana na ukweli kwamba anapambana na hisia za kunitamani zilizomzinduka usiku ule ndani ya gari.

Siku ya kumi na tano, nikiwa nimekaa sebuleni kwangu nimekata tamaa, simu ilitetemeka kwa ghafla. Jina "Kaka Kelvin" liliwaka kwenye kioo. Moyo wangu ulilipuka kwa furaha! Nilivuta pumzi ili nisifanye sauti yangu ionekane ina shauku kubwa sana, kisha nikapokea.

"Hello, Salma. Habari za siku tele mdogo wangu?" sauti yake ilikuwa ile ileโ€”tulivu na yenye ukarimu, kana kwamba hakuna kitu cha aibu kilichotokea kati yetu.

"Salama Kaka Kelvin... niko salama tu," nilijibu kwa unyonge wa kujitengenezea ili anihurumie.

"Poleni na majukumu mwaya. Naomba jioni ya leo tukutane pale Sea Cliff, kwenye ule mgahawa wa nje unaotazama bahari. Kuna jambo zuri sana nataka kukushirikisha na kuna zawadi yako nataka kukukabidhi. Saa kumi na moja jioni itafaa?"

"Sawa, nitakuja," nilijibu haraka kabisa kabla hajakata simu.

Nilizinduka pale pale. Akili yangu ilituma ujumbe mmoja tu: *Kelvin ameshindwa kuvumilia ukimya! Ananialika sehemu ya kishua na ya kimahaba kama Sea Cliff jioni kwa sababu anataka kuweka mambo sawa baada ya kukaa na hamu yangu kwa wiki mbili.*

Muda ule ule nilifungua kabati langu. Safari hii niliamua kwenda kimtego zaidi ili asipate pa kutokea. Nilichagua kigauni chepesi cha kamba (spaghetti strap) cha rangi ya maziwa, kilichokuwa kimeshika makalio yangu vizuri na kuacha mgongo wote wazi hadi kiunoni. Chini sikuwa nimevaa chupi; nilitaka tu upepo wa bahari ukipeperusha kigauni kile, ajue kabisa hakuna kizuizi chochote kati yangu na yeye usiku huu. Nilipaka mafuta ya kunogesha ngozi na kujifukiza manukato yangu yale yale ya vanilla yenye kuamsha hisia.

Saa kumi na moja kamili, bajaji iliniacha Sea Cliff. Niliingia eneo la mgahawa kwa madaha, nikitembea kwa pozi zilizokuwa zinasababisha wanaume waliokaa pale kugeuza shingo zao. Nilimwona Kelvin amekaa meza ya pembeni kabisa inayotazama mawimbi ya bahari. Alikuwa amevaa jinsi ya bluu na t-shirt ya mikono mifupi iliyobana vizuri kifua chake kipana na kuacha misuli ya mikono yake ikionekana kwa ufundi.

"Wow, kichuna wangu! Umependeza sana leo," Kelvin alisema akisimama na kunipiga kumbatio la kipekee. Mkono wake ulipita kwenye ule mgongo wangu uliokuwa wazi, na joto la kiganja chake lilifanya mwili wangu wote upate joto la ghafla la mahaba.

"Asante," nilinong'ona nikiwa namtazama kimahaba moja kwa moja kwenye macho yake.

Tulikaa na kuagiza vinywaji. Kelvin alikuwa anaongea kwa furaha kubwa sana, akicheka na kunisimulia dili jipya alilolipata lililomfanya asafiri. "Salma, kwanza kabisa chukua hii," alisema akisogeza bahasha nene ya kahawia mbele yangu. "Hii ni asilimia yako ya faida kwenye lile dili la ofisini, na nimeongeza na kiasi kidogo cha matumizi yako ya mwezi huu maana najua umekwama."

Niliipokea ile pesa, nikihisi jinsi Kelvin anavyozidi kuwa mwanaume kamili wa maisha yangu. Nilivuta kiti changu karibu naye zaidi, nikapitisha mguu wangu chini ya meza na kuanza kusugua paja langu kwenye mguu wake kwa siri, huku nikimtazama kwa macho ya kurembua.

"Kaka Kelvin... unajua jinsi gani nilivyokukumbuka? Huu ukaribu wako unanikosha sana," nilisema kwa sauti ya chini, ya mahaba, huku mkono wangu mmoja ukiwa juu ya meza umeanza kuchezea vidole vyake.

Kelvin alitazama mkono wangu, kisha akatazama jinsi mguu wangu unavyocheza na wake chini ya meza. Tabasamu lake lilipotea kwa sekunde moja, akavuta pumzi ndefu na kunikata jicho lililojaa msisitizo, akisogeza mguu wake pembeni ili kunikwepa.

"Salma, nilizani tulishaongea kuhusu hili jambo?" alisema kwa sauti ya chini ili watu wa meza nyingine wasisikie, lakini ikiwa na msisitizo mkali unaouma. "Mimi ni kaka yako. Na sifa kuu ya mwaliko wa leo ni kwa sababu kuna mtu muhimu sana anakuja hapa sasa hivi kuungana nasi, mtu ambaye maisha yangu yote yanamtegemea yeye."

Kabla sijaelewa maana ya maneno yake, Kelvin alitazama upande wa lango kuu la mgahawa na uso wake ukaangaziwa na tabasamu kubwa la dhati ambalo sijawahi kuliona tangu nifahamiane naye. Alisimama haraka sana kwenye kiti chake.

Niligizika na kugeuka kutazama kule anakotazama. Moyo wangu ulistuka na kuhisi baridi ya ghafla ikinitandika mwili mzima.

---

> **Katika Episode Inayofuata (Episode 6: Ugeni wa Mshtuko):** Mtu anayeingia mgahawani hapo anamfanya Kelvin asahau kila kitu na kukimbia kumlaki. Salma anabaki amepigwa na butwaa, huku kigauni chake cha mtego na ukosefu wa nguo ya ndani vikimgeuka kuwa dharau mbele ya ugeni huo mzito. Ni nani huyu anayekuja kupindua meza ya Salma? Usikose **Episode 6**!