Episode 14: Sina Msamaha
Juma aliamka asubuhi huku mwili ukimuuma kama amepigwa na rungu la kimasai. Akiwa bado anajinyoosha kwenye lile benchi la zahanati, alimwona kijana mmoja anakuja kwa kusitasita. Alikuwa ni yule rafiki yake wa zamani aliyewahi kumdhulumu simu yake ya tochi miaka miwili iliyopita.
Kijana yule alipiga magoti mbele ya Juma. "Juma ndugu yangu, nimekuwa nikiishi kwa tabu tangu nikuibie ile simu. Nimekuja unipe msamaha ili roho yangu itulie."
Juma alimtazama yule rafiki yake, kisha akajishika mifuko yake ambayo ilikuwa haina hata senti moja ya kununua maji ya kunywa. Alishusha pumzi ndefu na kumjibu kwa upole, **"Ushawahi kukosa kila kitu, hata ukiombwa msamaha unasema huna?"**
Yule rafiki alishangaa. "Unamaanisha nini Juma? Msamaha haununuliwi."
Juma akajibu, "Ndugu yangu, kwa sasa nimefulia kiasi kwamba hata hicho kitu kinachoitwa 'msamaha' kimeisha kwenye stoku yangu. Nimeishiwa hela, nimeishiwa chakula, nimeishiwa usingizi, na sasa nimeishiwa hadi huruma. Labda urudi keshokutwa nikiwa nimepata hata chai, naweza nikazalisha msamaha kidogo."
Yule kijana alibaki ameduwaa. Juma akanyanyuka na koti lake begani na kumuacha hapo hapo huku akisema, **"Huna hela halafu unajiombea maisha marefu, ukipewa hayo maisha marefu utakula nini?** Mimi hapa hata msamaha tu siwezi kuutoa maana sina nguvu ya kuusema."
Juma aliondoka akielekea mjini kati, huku akiona jinsi watoto wa kisasa wanavyobembelezwa mtaani, jambo ambalo lilimkumbusha machungu ya enzi zake za utoto.
---
**Kionjo cha Episode 15:** Juma anashuhudia mtoto wa kishua akigoma kunywa uji, anachambua tofauti ya malezi ya sasa na yale ya enzi zao ya "kubanwa pua." Usikose **Ep 15: "Uji na Katuni."**