✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 20: Deni la Damu na Sadaka ya Mahaba

Ule ufa uliotokea kwenye kioo kikuu cha mnara haukuwa wa kawaida; ulikuwa ni ufa wa kwanza katika ulimwengu wa kivuli. Kila sekunde ilivyokuwa inasonga, sauti ya ule mipasuko ilikuwa ikisikika kama kilio cha maumivu. **Anitha** alihisi baridi kali moyoni mwake alipomtazama mume wake.

**Bakari** alianza kubadilika. Kiganja chake alichokuwa amekishika Anitha kilianza kuwa angavu, kisha kikafifia na kuwa kama moshi wa fedha. Ule mwili wake wa shaba, wenye misuli na joto, ulikuwa unarudi kuwa picha tu ya kioni.

"Anitha... muda wangu wa kukaa nje ya kioo unaisha," Bakari alisema kwa sauti inayofifia kama mwangwi. "Mizimu inataka mwili wangu urudi kurekebisha ulimwengu wa kivuli uliovurugika."

Anitha alilia kwa uchungu, akijaribu kumkumbatia Bakari lakini mikono yake ilikuwa inapita katikati ya kifua cha Bakari kama inakamata hewa. "Hapana! Huwezi kuniacha mimi na mwanao! Nimepewa kila kitu, siwezi kurudi kuwa peke yangu!"

Ghafla, sauti ya radi ilivuma ndani ya kioo kilichopasuka: **"Ili binadamu aishi na kivuli milele, lazima damu ya nyama ichanganywe na roho ya kioo. Sadaka ni lazima, Anitha!"**

Anitha alimtazama mwanawe, **Kioo Jr**, aliyekuwa aking'aa kwa amani. Alijua hawezi kumtoa mwanawe. Alitazama kile kioo, kisha akamtazama Bakari ambaye sasa nusu ya mwili wake ulikuwa tayari umeshapotea.

"Bakari, kama huwezi kubaki duniani, basi mimi nitakuja huko!" Anitha alipiga kelele. Alichukua kipande cha kioo kilichokuwa kimevunjika sakafuni, akajichanja kiganja chake cha mkono wa kushoto, damu nyekundu na nzito ikachirizika.

Alikishika kile kioo cha mnara kwa kiganja chenye damu, na ghafla, umeme wa rangi ya zambarau uliwapiga wote. Anitha alihisi mwili wake ukivutwa kwa nguvu ya ajabu. Haikuwa maumivu ya kifo, bali ilikuwa ni hisia ya kuyeyuka.

Katika dakika hiyo ya mwisho ya mpito, Bakari alimvuta Anitha kwa mara ya mwisho. Akiwa nusu binadamu na nusu kivuli, Bakari alianza ufundi wa "Sadaka ya Mahaba." Alimshika Anitha kiuno, akamuinua juu huku miguu ya Anitha ikining'inia kati ya ulimwengu wa binadamu na ule wa kioo. Alimshindilia kwa ufundi wa "Mvunjiko wa Moyo," kila pigo likiwa na mchanganyiko wa damu na mwanga.

Anitha alipiga kelele ya raha ya mwisho: *"Bakari! Twende wote! Nizike ndani ya kioo chako!"*

Mlipuko mkubwa wa mwanga ulitokea. Jengo la Lux Relax lililojaa kioo lilitoa mwangaza ulioweza kuonekana mji mzima, kisha ghafla... *kimya.*

Asubuhi ilipofika, jengo lile lilikuwa limerudi kuwa gofu la zamani. Kuta hazing'ai tena, vito vya dhahabu vimepotea. Wapita njia walichuchumia na kuchungulia ndani ya Chumba Namba 07. Chumba kilikuwa tupu. Hakuna Anitha, hakuna Bakari, wala yule mtoto.

Lakini kitu kimoja tu kilibaki: Kile kioo cha mnara kilikuwa kimerudi kuwa kizima na safi kuliko wakati mwingine wowote. Ukikaribia kukitazama, huoni sura yako; unawaona Anitha na Bakari wakiwa wamekumbatiana kwenye bustani ya ajabu ya kioo, huku mtoto wao akicheza pembeni yao.

Wote wawili sasa ni wakazi wa upande wa pili. Wanawake wanaopanga kwenye chumba kile sasa wanasema, ukiwa uchi mbele ya kioo hicho na ukakata mauno kwa ufundi, unahisi mikono ya ajabu ikikupapasa na sauti ikikufundisha ufundi wa "Kioo cha Gesti."

**— MWISHO —**