✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 27: RISASI ZA USIKU NA KIFO CHA DALALI

Milio ya risasi ilipasua anga la usiku wa manane pale nje ya gesti. "Pua! Pua! Pua!" Askari walikuwa wakiwafyatulia risasi wale madalali wawili waliokuwa wanajaribu kukimbilia kwenye kichaka cha jirani. Nilichungulia kupitia dirisha la gari la polisi nikiwa nimejifunika shuka, moyo ukiwa unanidunda kwa kasi.

Mmoja wa wale madalali alipigwa risasi ya mguu na kuanguka chini akipiga kelele za maumivu, lakini yule wa pili alifanikiwa kutokomea gizani. Bosi alikuwa amepiga magoti pembeni ya gari lingine la polisi, akilia na kuomba msamaha, huku akidai kuwa yeye ni mfanyabiashara halali.

"Nyamaza wewe mzee mnafiki! Hizi pasipoti tano za hawa binti nimezikuta ofisini kwako ni za nini?" Askari mmoja alimfokea huku akimzaba kibao cha sikio.

Mama Shua alikuja kusimama mbele ya gari nililokuwemo. Alikuwa anatazama ile gesti kwa dharau kubwa. "Marina, leo nimefunga rasmi hili pango la shetani. Lakini usizani safari yako imeishia hapa. Inabidi uende kutoa ushahidi mahakamani ili huyu mzee asitoke kamwe," aliniambia kwa sauti ya baridi.

Tulipelekwa kituoni, na safari hii sikutupwa selo. Nilipewa chumba kidogo cha mapumziko huku nikipewa chai na mkate. Nilikaa pale nikiwaza maisha yangu. Nilikumbuka zile laki saba zangu nilizokuwa nimezificha kwenye sidiria na nyingine kwenye chupi kabla ya bosi kunivamia. Nilizitoa na kuziangalia; zilikuwa zimejaa jasho na harufu ya unyevu.

"Hizi pesa zimenigharimu utu wangu," niliwaza huku nikiangua kilio cha uchungu.

Siku iliyofuata, habari zilikuwa zimeenea mji mzima. Kichwa cha habari kwenye magazeti kilisema: **"MTANDAO WA KUUZA BINADAMU WANASWA GESTI, MBUNGE NA MASHUHURI WAHUSISHWA."** Niligundua kuwa mchezo ulikuwa mkubwa kuliko nilivyodhani. Juma alikuwa gerezani, bosi alikuwa gerezani, na mimi nilikuwa shahidi namba moja.

Baada ya wiki mbili za mahojiano na kesi, Mama Shua aliniita ofisini kwake. "Marina, kesi imeisha. Bosi wako amehukumiwa miaka 30 jela. Sasa, unataka kufanya nini na maisha yako? Sitaki kukuona tena barabarani."

"Nataka kurudi kijijini kwa mama yangu," nilimjibu kwa unyonge. Nilihisi nimechoka na mji, nimechoka na wanaume, na nimechoka na maisha ya mkato.

Mama Shua alinipa bahasha yenye laki tano nyingine. "Hii ni zawadi yangu kwako kwa ujasiri wa kutoa taarifa. Nenda kijijini katusaidie mama yako, na ukaanze maisha mapya. Lakini kumbuka, siri ya yote yaliyotokea hapa ibaki moyoni mwako."

Niliondoka mjini nikiwa na jumla ya milioni moja na laki mbili. Nilipofika kijijini, nilimkuta mama yangu akiwa amedhoofika kwa ugonjwa. Aliponiona alilia kwa furaha, akidhani mwanaye amepata kazi ya maana mjini. Nilishindwa kumwambia ukweli kuwa pesa nilizompa zilitokana na kuchezewa na wanaume, kunyonywa papuchi, na kufungwa pingu.

Lakini maisha ya kijijini hayakuwa rahisi kama nilivyodhani. Baada ya mwezi mmoja, nilianza kuhisi kichefuchefu na kizunguzungu. Nilijaribu kujizuia lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Siku moja asubuhi nikiwa naenda kisimani, nilianguka chini na kupoteza fahamu.

Nilipozinduka, nilimkuta muuguzi wa kijijini akinitazama kwa masikitiko. "Marina, una ujauzito wa miezi miwili. Na kibaya zaidi... una maambukizi ya virusi vya UKIMWI."

Dunia ilizunguka. Nilikumbuka bosi, nikamkumbuka yule fundi wa laki moja, nikamkumbuka Juma, na yule mbunge. Nani kati yao alikuwa amenipa zawadi hii ya kifo?

---
**Inaendelea Sehemu ya Mwisho (Final Episode)...**