✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 1: Jirani Mpya, Siri Mpya

Maisha yangu katika mtaa huu wa utulivu yalikuwa ya upweke, lakini yenye amani. Nyumba yangu ilikuwa ndefu, kiasi cha kuniwezesha kuchungulia ndani ya fensi za majirani zangu wa nyuma. Siku hiyo, nikiwa dirishani, niliona malori ya mizigo yakiegeshwa kwenye nyumba iliyokuwa wazi kwa muda mrefu. Familia mpya ilikuwa inahamia.

Moyo wangu ulinisukuma kwenda kuwasalimia. Kama ilivyo desturi ya ukarimu, nilinunua mkate mkubwa na kuelekea huko. Nilikutana na mwanamke mrembo, **Jenifer**, ambaye alikuwa anashusha vyombo.

"Karibuni sana mtaani," nilimwamkia kwa tabasamu.

"Ahsante sana, naitwa Jenifer," alijibu huku akipokea mkate ule.

Mazungumzo yetu yalinoga, lakini ghafla mlango wa gari ulifunguka na akatoka mkaka mtanashati, mrefu, na mwenye kifua kilichojazia. Alikuwa anaitwa **Michael**. Nilijikuta nikimtaja kama "shemeji," lakini Jenifer alicheka kicheko chenye uchungu kidogo.

"Huyu si mume wangu tena, Zakia. Tumeachana, ingawa tuna mtoto mmoja anaitwa Enock. Nimekuja tu kumsaidia kuhamia," Jenifer alieleza.

Lakini jambo moja lilinitia shaka. Jenifer alikuwa akitembea kwa shida sana, kama mtu aliyeteguka kiuno au mwenye maumivu makali ya ndani. Alipokuwa akitembea, macho yake yalikuwa yanamtazama Michael kwa namna fulaniβ€”siyo ya mapenzi, bali kama ya hofu na mshangao.

"Jenifer, mbona unatembea hivyo? Unaumwa kiuno?" Nilishindwa kuzuia udadisi wangu.

Jenifer alimtazama Michael, kisha akamtazama chini ya mkanda wake wa suruali, akashusha pumzi na kusema, "Hali hii ndiyo chanzo cha mimi na Michael kuachana. Utakuja kuelewa mbeleni, Zakia."

Nilirudi kwangu nikiwa nimejaa maswali. Michael alikuwa mtanashati kupita kiasi, lakini maneno ya Jenifer yaliacha alama ya hofu moyoni mwangu. Je, kuna siri gani imejificha nyuma ya ule mtanashati wa Michael?

---
**Je, unahitaji nini kitafata Sehemu ya 2?**