✦ Matangazo ✦

Story Tamu

Episode 17

UAMUZI WA KAZI MPYA NA JARIBIO LA KWANZA LA UJAMZITO

Maisha ya kuishi pamoja chumba kimoja yalianza kwa mahaba mazito na utulivu wa ajabu. Chumba cha Joel kilibadilika kabisa; kilijaa harufu nzuri ya marashi ya Nuru, nguo zake safi na tabasamu lake la kila asubuhi. Hata hivyo, Joel alijua fika kuwa majukumu yameongezeka. Kutunza mwanamke mwenye ujauzito mchanga na kujiandaa na mtoto kulimfanya aanze kutafuta michongo ya ziada ya fedha ili kuongeza kipato chake cha kila siku.

Asubuhi hiyo, Joel aliamka mapema, akambusu Nuru aliyekuwa bado amelala uchi wa mnyama chini ya mashuka na kumwambia: "Mke wangu, naenda mjini kufuatilia malipo ya kazi yangu na kuangalia mchongo mpya. Nitarudi mapema mchana."

Nuru alitabasamu kwa mahaba, akimvuta Joel na kumpa busu zito la mdomoni. "Nenda salama mume wangu... mimi na mwanao tunakusubiri."

Majira ya saa sita mchana, Nuru akiwa peke yake chumbani akifanya usafi mdogo, ghafla alihisi mchomo mkali na wa kutisha chini ya kitovu chake. Maumivu hayo yalimkata tumbo kwa kasi ya ajabu, yakimfanya adondoshe deki chini na kujishika tumbo huku akipiga kelele ya maumivu: "Aiiih... Mungu wangu!"

Mwili wake wote ulivuja jasho la baridi kwa sekunde chache. Alipogeuka na kutazama chini kwenye mapaja yake, aliona mchirizi mdogo wa damu ukianza kushuka taratibu kuelekea miguuni. Hofu kubwa ya kupoteza mimba ya Joel ilimkamata nafsi yake. Alidondoka chini sakafuni karibu na kitanda, akilia kwa uchungu na kushika tumbo lake.

Mama Chiku aliyekuwa akipita nje alisikia kilio hicho cha chini. Alisogea mlangoni na kupiga hodi kwa wasiwasi: "Nuru! Nuru kuna nini huko ndani?"

Nuru, akitumia nguvu zake zote za mwisho, alitambaa hadi mlangoni na kufungua komeo. Mama Chiku alipomuona Nuru akiwa amejishika tumbo na damu ikimwagika miguuni, mshtuko ulimshika na kusahau udaku wote wa nyuma. Alimsaidia kumweka kitandani na kumpigia Joel simu ya dharura.

Joel alipopokea taarifa hizo akiwa mjini, akili ilimruka! Alikimbia kwa spidi ya hatari na kupanda bodaboda iliyomrudisha uchochoroni kwa dakika chache tu. Alipoingia chumbani na kumkuta Nuru akitweta kwa maumivu kitandani, Joel alipiga magoti pembeni yake huku machozi yakimlenga.

"Nuru! Nuru mpenzi wangu!" Joel alinong'ona kwa sauti iliyotetemeka, akimshika mkono na kupanguza jasho usoni mwake.

Nuru alimwangalia Joel kwa macho yaliyojaa machozi na mahaba mazito: "Joel... mwanetu... simamia usiruhusu mwanetu aondoke..."

Joel hakusubiri msaada mwingine. Alimnyanyua Nuru juu kwa mikono yake imara, akamfunga kanga vizuri na kumkimbiza kwenye zahanati ya karibu iliyopo mtaani hapo.

Daktari alifanya uchunguzi wa haraka na kumchoma Nuru sindano ya kutuliza uzazi na kumpa dawa za kuzuia damu. Baada ya masaa mawili ya hofu na maombi mazito, Daktari alitoka nje na kutabasamu mbele ya Joel.

"Kijana, tuliza roho yako. Mimba iko salama kabisa," Daktari alisema. "Ilikuwa ni mshtuko mdogo wa mfuko wa uzazi kutokana na uchovu au kufanya kazi nzito. Anahitaji mapumziko ya kutosha na mahaba mwanana bila msongo wa mawazo."

Joel alishusha pumzi ndefu ya furaha na kumshukuru Mungu. Alingia chumbani alimokuwa amelazwa Nuru, akamkumbatia kwa upole mkubwa na kumpiga busu mwanana kwenye paji la uso.

Usiku huo, baada ya kuruhusiwa na kurudi chumbani kwao, Joel alimweka Nuru kitandani kwa uangalifu mkubwa. Nuru alipokuwa amejilaza kwa utulivu, alimshika Joel mkono na kumvuta kitandani.

"Joel... nataka unifanye nishahidi kuwa mwanetu yuko salama," Nuru alinong'ona kwa sauti mwororo iliyotawaliwa na hamu na amani mpya.

Joel alimvua Nuru nguo zake kwa upole mno. Alipanda juu yake taratibu sana, akiweka uzito wake pembeni. Alitumbukiza uume wake wa moto ndani ya Nuru kwa nhwendo wa taratibu na mwororo kuliko siku zote—chok!

Nuru alishusha pumzi ndefu ya raha—Aaaah Joel...—akifunga macho na kuzungusha kiuno chake kwa miondoko ya taratibu na ya ndani kabisa. Joel alipiga shughuli kwa mahaba ya dhati na umakini mkubwa, kila msukumo ukileta utamu wa pekee na amani iliyowafikisha wote wawili kileleni kwa pamoja kwa utulivu mkubwa wa usiku huo.


UTANGULIZI WA EPISODE INAYOFUATA:

EPISODE 18: KUTEMBELEWA NA NDUGU NA SHARTI LA NDOA
Wakati maisha yao yakirudi kwenye amani na furaha, dada yake mkubwa na Nuru anawasili ghafla kutoka mkoani kuja kumwangalia mdogo wake baada ya kusikia habari za ujauzito huo. Dada huyo anapogundua Nuru anaishi na kijana bila ndoa wala baraka za wazazi, anatoa sharti zito linalomweka Joel kwenye mtihani mkubwa wa kifedha na kifamilia. Je, Joel ataweza kukabili sharti hilo ili kumweka Nuru halali? Usikose Episode 18!