✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 8: UKURASA MUPYA NA MAUMIVU YA URAIANI

Mwanga wa jua la asubuhi ulipenyeza kwa ustadi kupitia pazia jepesi la chumba cha ghorofa cha Suzana. Baada ya tukio zito la Jumapili iliyopita kanisani, mji mzima ulikuwa ukiongea kuhusu ukweli uliowekwa wazi. Mchungaji Eliya na Mzee Zakaria walikuwa wamejifungia ndani kwa aibu, huku uongozi mpya wa muda wa waumini ukichukua hatua za kusafisha kanisa.

Amani na Suzana walikuwa wamelala kitandani, miili yao ikiwa imekumbatiana kwa mahaba na utulivu mkubwa ambao hawakuwa naowatangu siku nyingi. Amani alikuwa akipitisha vidole vyake kwenye nywele za Suzana huku akimtazama kwa macho yaliyojaa shukrani na mapenzi ya dhati.

"Suzana wangu," Amani alinong'ona kwa sauti ya chini na ya upendo. "Kila kitu kilitokea kwa sababu. Kama siyo wewe kuwa jasiri na kunifungua macho, pengine ningebaki kwenye mtego wa kuwaabudu wanadamu waliovaa ngozi ya kondoo."

Suzana alitabasamu na kuinua kichwa chake kifuani mwa Amani. Alimshika Amani shingoni na kumpiga busu zito la mdomoni lililowasha moto mpya mwilini mwao. Suzana alipanda juu ya Amani taratibu, akipitisha mikono yake kwenye kifua cha Amani kilichojengeka vyema. Amani alimshika Suzana kiunoni na kumvuta chini kwa hamu. Walifanya mapenzi kwa utulivu na hisia za dhati kabisa za mume na mke wa baadaye, wakijaza chumba kile kwa miguno ya furaha na amani ya nafsi.

Baada ya mapumziko hayo ya asubuhi, wawili hao walikaa mezani kupata kifungua kinywa na kupanga mustakabali wa biashara zao. Walikubaliana kuunganisha nguvu zao za kiuchumi: duka la vifaa vya kielektroniki la Amani na mtandao wa migahawa na maduka ya jumla ya Suzana.

Hata hivyo, uraiani mambo hayakuwa rahisi kabisa. Licha ya kufichua uovu na kurudisha Milioni 50 zote kanisani, baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa kidini na marafiki wa zamani wa Mchungaji Eliya walianza kueneza maneno ya shombo mtaani. Walimyooshea Suzana kidole wakimwita "binti wa klabu aliyempotosha kijana wa kanisa", huku Amani akionekana kama msaliti aliyedhalilisha madhabahu.

Siku chache baadaye, Amani alipokuwa dukani kwake, kundi la vijana waliotumwa na ndugu wa Mzee Zakaria lilifika na kujaribu kumfanyia fujo na kuvunja vioo vya duka lake kwa hasira za kuasifiwa kwa mzee wao.

Amani alisimama kidete bila woga wowote, akijua wazi kuwa vita ya ukweli daima ina gharama zake. Lakini swali kubwa lilikuwa: Je, maadui hawa wa siri watakubali kushindwa kiurahisi hivyo au wanapanga njama mbaya zaidi za kulipiza kisasi dhidi ya maisha na biashara za Amani na Suzana?

---

**UTANGULIZI WA EPISODE 9: NJAMA ZIKUSANYAZO GIZANI**
Wakati Amani na Suzana wakijiandaa kurasimisha mahusiano yao na kufunga ndoa, Mzee Zakaria na Mchungaji Eliya wanakutana kwa siri maeneo ya uswahilini kupanga mpango mchafu wa kuharibu biashara za Suzana na kumfanyia Amani jambo la kutisha. Je, mpango huo wa kisasi utafanikiwa? Usikose Episode ya 9!