✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 21: Mazishi ya Laana na Folda ya Mwisho Fungwa

Kuning'inia kwa mwili wa Asha Machozi mbele ya lile bango la saluni kulileta kiama cha kisaikolojia mtaani Shaurimoyo. Watu walijaa kwa mamia, wakiwa wamemviringizia duara, lakini hakuna mtu aliyethubutu kusogea karibu kuushusha ule mwili wa mifupa. Kila mmoja alikuwa akitazama kwa uoga na unyanyapaa mkuu, wakinyoosha vidole kwenye yale malengelenge yaliyofunika sura yake iliyokuwa nembo ya urembo mtaani hapo.

Sudi mbea alikuwa amesimama mbele kabisa akitikisa kichwa. "Ona sasa! Huyu ndio Asha aliyekuwa anaringa mtaani kwetu. Kumbe alishaoza kwa ngoma ya Brayan, leo ameamua kujinyonga hapa ili kila mtu ajue siri yake!" sauti ya Sudi ilijaa kejeli iliyochanganyika na hofu.

Gari la polisi lilifika baada ya saa mbili na kuushusha mwili ule uliokuwa ukitoa harufu ya ugonjwa. Walimtupa nyuma ya karandinga bila heshima yoyote, kama mzoga wa mnyama aliyekufa kwa laana. Hakuna ndugu aliyemlilia Asha, na wazazi wake walijifungia ndani kwa aibu, wakikataa hata kuupokea mwili huo kwa ajili ya mazishi ya kifamilia. Alizikwa siku hiyo hiyo kwenye makaburi ya umma, hatua chache kutoka pale lilipofukiwa jeneza la Brayan.

Wakati Asha akizikwa kwa laana hiyo mtaani, kule Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Zuena naye alikuwa anafikia sentensi ya mwisho ya kitabu chake cha maisha. Baada ya siku 101 za mateso mazito, mapafu na ubongo wake vilikuwa vimeshaelemewa kabisa na sumu ya kaswende na virusi.

Majira ya saa kumi na moja jioni, jua la jiji la Dar es Salaam likiwa linaanza kuzama, macho ya Zuena yalifunguka kwa tabu sana. Alitazama dari la chumba chake cha upweke. Alihisi ule unyevu wa mwisho wa maisha ukimtoka. Kwa mara ya mwisho, alitamani kusikia sauti ya Mzee Mfaume akimwita "mke wangu," lakini chumba kile kilikuwa na ukimya wa makaburi.

*Beep............................................*

Mashine ya moyo ilitoa mlio mrefu wa kunyooka. Zuena akakata roho akiwa peke yake, bila mtu wa kumfuta machozi ya mwisho ya majuto yaliyokuwa yanachuruzika kwenye mashavu yake yaliyonyauka.

Siku mbili baadaye, ndani ya Ofisi kuu ya Upelelezi ya Kituo cha Polisi Shaurimoyo, Inspekta mkuu alikuwa amekaa kwenye kiti chake cha ngozi, uso wake ukiwa na uchovu mwingi. Mbele yake, juu ya meza, kulikuwa na faili kubwa lililoandikwa *'Operation Orodha ya Kifo: Brayan na Wenzake'*.

Pembeni ya lile faili, ilikuwa imelala ile Flash-Diski nyekundu ya GB 128β€”ile bima ya siri ambayo Brayan aliificha chini ya godoro lake ikawa chanzo cha anguko la mtaa mzima.

Inspekta alishika ile flash, akaitazama kwa masikitiko makubwa. "Kijana mmoja mwenye tamaa, kamera moja, na weledi mbovu, vimefuta maisha ya wanawake nusu ya mtaa. Hakuna mshahidi aliyebaki hai kutoa ushahidi mahakamani. Kila folda sasa haina mmiliki," alisema akinong'ona.

Aliichomeka ile flash kwenye kompyuta kwa mara ya mwisho. Folda za akina Zuena, Asha Machozi, Mwajuma, na Tausi zilifunguka kwenye kioo. Alibonyeza folda zote kwa pamoja, akabonyeza kitufe cha *'Delete'*, kisha akathibitisha kwa *'Permanently Delete'*.

Kioo cha kompyuta kikabaki tupu. Folda zote za siri, video zote za ngono, na kumbukumbu zote za unyevu wa uzinzi uliomwagika ndani ya lile geti jeusi zilifutwa rasmi mikononi mwa sheria.

Inspekta alifunga lile faili, akapiga muhuri mkubwa mwekundu uliandikwa: **CASE CLOSED (KESI IMEFUNGWA)**.

Mtaa wa Shaurimoyo ulibaki na kovu lisilofutika. Lile geti jeusi lililovunjika lilikuja kusingizwa na kupigwa mnada, na hakuna kijana wala mzee aliyetamani kupita karibu na eneo lile tena. Ikawa ni fundisho la milele kwa mtaa mzima kuwa; uzuri wa sura, ushauri wa kipuuzi wa marafiki, na utamu wa dakika kumi na tano wa ngono zembe, unaweza kugeuka kuwa kitanzi cha nondo kinachopeleka kizazi kizima kwenye kaburi la aibu na upweke mkuu.

---

**MWISHO WA SIMULIZI.**