Episode 7: Siri ya Uhaini wa Mapenzi
Sam alishusha pumzi ndefu baada ya kunilisha kijiko cha tano cha chocolate. Aliniangalia machoni, safari hii hakuwa na lile tabasamu lake la kawaida; alikuwa na sura ya huzuni iliyochanganyika na hasira ya ndani kwa ndani.
“Tedy, unanitazama hivi nina umri wa miaka thelathini,” Sam alianza kusimulia. “Huko nyuma nilikuwa na malengo makubwa sana kwamba nitaoa kabla ya kuzidi umri huu. Katika pita pita zangu kazini, nilimwona Saraphina kama mwanamke anayenifaa. Nilivunja mipaka ya uboss, nikamweleza hisia zangu na malengo yangu ya ndoa. Hakusita, alinikubalia.”
Moyo uliniuma kidogo kusikia kuwa walikuwa na mpango wa ndoa, lakini nikaendelea kusikiliza.
“Tulipanga kufunga ndoa mwaka huu,” Sam aliendelea. “Lakini miezi sita iliyopita, nikiwa ofisini, nilienda ofisi ya Hussein kumtafuta. Kabla ya kufungua mlango, nilisikia sauti za Saraphina na Hussein wakicheka na kupanga mipango ya ajabu. Hussein na Saraphina walikuwa kwenye huba zito tangu zamani! Kumbe kunikubalia kwangu ilikuwa ni shinikizo la Hussein ili aniole, nichote pesa nyingi kampuni, kisha baada ya miaka mitano adai talaka tugawane mali pasu kwa pasu, kisha aende kuanza maisha na Hussein wake!”
Nilibaki mdomo wazi. "Maskini Sam! Kwahiyo ulijua kila kitu?"
“Ndio Tedy. Tangu siku hiyo nikajifanya mjinga, nikataka kuona ukomo wa unafiki wao. Ndio maana nilipokuona wewe, nilihisi moyo wangu umepata kimbilio la kweli. Wewe huna hila, una upendo wa dhati.”
Nilimshika Sam mkono. “Umelijua kosa lako hapo Sam? Kosa ni kutokumwambia kuwa unajua ukweli. Mpaka sasa anajiamini kuwa yeye ni mkeo mtarajiwa, ndio maana anapata nguvu ya kunishambulia. Unapaswa kumaliza huu mchezo haraka.”
Sam alitabasamu kidogo na kunikumbatia. “Umenishauri jambo la hekima sana mke wangu mtarajiwa. Nitamaliza hili jambo kesho ofisini.”
Tukiwa bado tumekumbatiana, simu ya Sam ilianza kuita kwa nguvu. Aliiangalia... alikuwa ni Hussein. Sam alipokea na kuiweka kwenye *loudspeaker*.
“Boss! Boss kimbia haraka!” Sauti ya Hussein ilikuwa ikitetemeka kwa hofu. “Saraphina amekunywa sumu hapa nyumbani kwake! Anasema usipokuja kumuokoa anakufa sasa hivi kwa ajili yako!”
Sam alishtuka na kusimama ghafla. Alinitazama kwa macho ya huruma na hofu. “Tedy, inabidi niende. Hata kama simpendi, ni binadamu mwenzangu, siwezi kumuacha afe!”
“Usiende Sam! Huu ni mtego mwingine!” nilimkataza kwa sauti kali, nikihisi kuna jambo baya linaenda kutokea.
“Nitarudi haraka mpenzi, nakuahidi,” Sam alisema huku akichukua funguo za gari na kukimbia kuelekea nje.
Nilibaki sebuleni peke yangu, moyo ukinidunda kwa kasi. Sikuwa na amani kabisa. Baada ya nusu saa, nilisikia kishindo kikubwa cha simu yangu ikiita. Ilikuwa ni namba ngeni.
“Halo, huyu ni Tedy? Kuna gari limepata ajali mbaya maeneo ya kuelekea Mikocheni... dereva amejikata vibaya na gari limepinduka. Tumekuta namba yako kwenye simu yake kama 'My Everything'...”
Nilihisi dunia inazunguka. Sam amepata ajali?
---
**Inaendelea Sehemu ya 8...**