✦ Matangazo ✦

πŸ“– Story Tamu

Episode 10: Mtego wa Video ya Giza

Sam alichukua simu yake kwa mkono uliokuwa bado unatetemeka kidogo. Alifungua ile video iliyotumwa na Hussein. Macho yake yalipanuka kwa mshtuko, na ghafla akawa mweupe kama karatasi. Alinitazama mimi, kisha akaitazama simu, kisha akainama chini kwa unyonge.

"Kuna nini Sam? Mbona umabadilika ghafla?" niliuliza huku nikijaribu kukaa vizuri kitandani licha ya maumivu ya kidonda cha figo.

Sam alinikabidhi simu bila kusema neno. Kwenye video ile, nilimwona kaka yangu (yule aliyenifukuza Dar) akiwa amekaa kwenye kiti, amefungwa kamba mikono na miguu, na uso wake ukiwa umejaa damu. Pembeni yake alisimama Hussein akiwa na bastola.

"Sikia wewe Sam," sauti ya Hussein ilisikika kwenye video. "Unajua fika kuwa huyu kaka wa Tedy ana deni la kampuni la milioni hamsini alizozichezea kipindi kile akiwa mhasibu msaidizi. Kama unataka huyu bwana aendelee kupumua, na kama unataka Tedy asijue uchafu wa kaka yake, basi utie saini fomu hizi za kukabidhi asilimia arubaini za hisa za kampuni kwa Saraphina. Ukikataa, kaka mtu anakufa, na Tedy atajua kuwa kaka yake ni mwizi!"

Nilihisi dunia inazunguka. Kumbe kaka yangu alikuwa mwizi wa kampuni ya Sam? Ndio maana alikuwa mkali kwangu na alitaka niondoke Dar haraka ili nisigundue ukweli? Naona aibu! Aibu ya kaka yangu ilikuwa ni aibu yangu pia.

"Sam, naomba unisamehe," nilisema huku nikilia kwa kwikwi. "Sikujua kama kaka yangu amefanya unyama huu kwako. Naomba usitoe hisa zako, ni kheri mimi niondoke hapa nikafe na aibu hii."

Sam alinivuta na kunikumbatia kwa nguvu. "Tedy, kosa la kaka yako siyo kosa lako. Na hizi hisa siyo kitu mbele ya maisha ya binadamu na mbele ya pendo lako kwangu. Umepoteza figo kwa ajili yangu, mimi nitashindwa nini kutoa karatasi za kampuni?"

Sam alimpigia Hussein simu papo hapo. "Hussein, nitafanya unachotaka. Lakini usimguse huyo mtu. Tukutane ofisini kesho asubuhi."

Siku iliyofuata, licha ya kuwa bado wagonjwa, tuliondoka hospitalini kwa siri na kuelekea ofisini. Hussein na Saraphina walikuwa wamekaa kwenye kiti cha mikutano wakisubiri kwa ushindi. Walikuwa na tabasamu la kishetani.

"Karibuni wapendanao," Saraphina alizungumza kwa kejeli. "Saini hapa Sam, na kila kitu kitaisha."

Sam alichukua kalamu. Lakini kabla hajaweka saini, mlango wa ofisi ulifunguka kwa kishindo. Polisi wanne waliongozana na mzee mmoja mwenye heshimaβ€”Mzee Kavishe, mmiliki mkuu wa kampuni aliyekuwa anaishi Canada, ambaye Sam alikuwa amempigia simu usiku kucha kumweleza hali halisi.

"Hussein na Saraphina, mchezo wenu umeishia hapa," Mzee Kavishe alizungumza kwa sauti ya mamlaka. "Nimefuatilia mienendo yenu kwa muda mrefu kupitia kamera za siri (CCTV) nilizozificha ofisini kwangu ambazo ninyi hamzijui. Tukio la kumteka kaka wa Tedy limerekodiwa pia na GPS ya gari lenu imewaumbua."

Hussein alijaribu kutoa bastola, lakini polisi walikuwa na kasi zaidi. Walimuwahi na kumdhibiti chini. Saraphina alianza kupiga kelele na kuomba msamaha, akijifanya kuzimia, lakini safari hii hakuna aliyemhurumia.

Kaka yangu aliokolewa na kufikishwa ofisini akiwa anatetemeka. Aliponiona, alianguka miguuni pangu na kulia. "Tedy, nisamehe! Tamaa ya mke wangu ndiyo ilinituma kuiba, na hawa watu walinitumia kama chambo."

Sam alimsimamisha kaka na kumwambia, "Nitakusamehe deni lako kwa sharti moja; rudi kijijini katusaidie maandalizi ya harusi yangu na mdogo wako. Sitaki kukuona mjini tena mpaka utakapojitambua."

Mzee Kavishe alinitazama mimi kisha akamtazama Sam. "Sam, umepata mwanamke wa dhahabu. Na kwakuwa umekuwa muaminifu hata katika hatari, kuanzia leo nakuongezea umiliki wa kampuni kwa asilimia ishirini nyingine kama zawadi ya harusi."

Tedy na Sam tulitazamana na kutabasamu. Maumivu ya kidonda changu cha figo yalionekana kutoweka kwa furaha ile. Hatimaye, giza lilikuwa limeondoka na alfajiri mpya ilikuwa imeanza.

"Tedy," Sam alinong'ona sikioni mwangu. "Sasa ni zamu yetu kwenda Songea. Nataka dunia ijue kuwa mimi ni Boss, lakini wewe ndiye Boss wa moyo wangu."

---
**Inaendelea Sehemu ya 11...**