✦ Matangazo ✦

📖 Story Tamu

Episode 3: Sauti ya Dada na Wingu la Mashaka

Ilikuwa ni jioni moja ya mwezi wa tano mwaka huu. Nilikuwa nimetoka tu kwenye mihangaiko yangu ya kawaida ya kila siku, nikiwa na mpango wa kuwahi nyumbani kama kawaida yangu ili nile chakula cha jioni pamoja na mke wangu na wanangu. Ghafla, simu yangu ilivibrate mfukoni. Nilipoitoa, niliona ni jina la dada yangu mkubwa, Asha.

"Assalamu Alaykum, kaka yangu," sauti ya dada ilisikika upande wa pili, lakini haikuwa na ule msisimko na kicheko chake cha kawaida. Ilikuwa sauti nzito na yenye kusita.

"Alaykum Salaam, dada Asha. Salama? Mbona sauti yako iko tofauti?" nilimuuliza kwa shtuko kidogo.

"Kaka, upo wapi kwa sasa? Kuna jambo muhimu sana nataka niongee na wewe hapa nyumbani kwangu. Tafadhali, fanya kila uwezalo uje sasa hivi kabla hujenda kwako," alisema, na kabla sijauliza swali lolote, akakata simu.

Moyo wangu ulianza kwenda mbio. Niligeuza usukani wa usafiri wangu na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa dada Asha. Nilipofika, nilimkuta amekaa sebuleni peke yake, uso wake ukiwa umekunjamana kwa mawazo mazito. Hata glasi ya maji aliyonisogezea haikuwa na ladha kwangu.

"Dada, una nini? Kuna tatizo gani limetokea kwenye familia?" nilimuuliza kwa shauku.

Dada Asha alivuta pumzi ndefu, akajisogeza karibu nami na kunishika mkono. "Kaka yangu, nakuomba uniwie radhi kwa nitakachokuambia. Nimekaa na hili jambo kwa muda mrefu nikiwa nalia peke yangu, lakini nimeona kama nikiendelea kunyamaza, nitakuwa nakusaliti wewe kama damu yangu."

Alichelewa kidogo kuendelea, akameza mate, kisha akashusha lile bomu: "Kuna maneno mazito sana yanaendelea mtaani na yameshafika hadi kwenye familia yetu. Kaka... huyo mkeo Subira unayeishi naye na kumsifu kila siku, kabla hujamuoa mwaka 2020, alishawahi kuzaa mtoto tayari. Na huyo mtoto kwa sasa yuko Darasa la Nne huko anakoishi na baba yake mzazi."

Nilihisi kama chumba kizima kimegeuka juu chini. Damu ilipanda kwa kasi hadi kichwani, masikio yangu yakaanza kupiga kelele *bzzzz*. Nilimkodolea dada macho huku nikitetemeka kwa hasira.

"Dada, una wazimu gani huu?! Unajua unachokiongea lakini?" nilimfokea, nikisimama kutoka kwenye kochi. "Subira nimemuoa mimi kwa mikono yangu! Nilimtoa bikira mimi mwenyewe, damu niliona kwa macho yangu mnyanduko wa kwanza! Unasemaje ana mtoto wa darasa la nne? Huu ni ushetani unataka kuniharibia ndoa yangu kwa wivu wenu!"

"Kaka, tulia! Mimi ni dada yako..." alijaribu kunishika mkono, lakini nilimkwepa.

"Sitaki kusikia upuuzi huu! Mwanamke aliyezaa atakuwaje bikira? Hizo ni chuki zenu tu mtaani!" Nilitoka nje ya nyumba yake kwa hasira kali, nikajibwiza kwenye usafiri wangu na kuondoka kwa kasi.

Nikiwa njiani kurudi nyumbani kwangu, akili yangu ilikuwa vurugu tupu. Nilikuwa nimekasirika, lakini ndani ya ile hasira, wingu jembamba la mashaka lilianza kujipenyeza moyoni mwangu. Kila nikikumbuka ule usiku wa kwanza, damu, na kubana kwa Subira, nilijaribu kujiaminisha kuwa dada yangu alikuwa anasema uongo. Nilifika nyumbani nikijitahidi kuficha hasira zangu, lakini picha ya Subira ilianza kubadilika taratibu machoni mwangu.

---

**Utangulizi wa Episode inayofuata:**
Katika **EPISODE 4: Maneno ya Chini kwa Chini na Mshtuko wa Subira**, tutaona jinsi nilivyojitahidi kulipotezea hili suala, lakini maneno ya mtaani yalivyoendelea kuvuma chini kwa chini hadi nikaamua kumtonya mke wangu kwa mara ya mwanza, na majibu yake ya mshtuko yaliyonipa amani ya muda mfupi. Usikose!